Afisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA, Bi. Marion Moore (katikati) akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) juu ya bidhaa mpya ya mkopo maarufu kama ‘Executive Loan’, jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Pamoja naye, kushoto ni Meneja Mauzo Kanda Bw. Haule Stephen na Mshauri Mkuu wa masoko Bw. Andrew Omusambayi.

TAASISI ya kifedha, Faidika imezindua bidhaa mpya ya mkopo maarufu kama ‘Executive’ inayolenga kuwezesha upatikanaji rahisi wa mkopo usiokuwa na dhamana kwa wafanyakazi wa serikalini wa mpaka shilingi milioni 30. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Afisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA, Bi. Marion Moore alisema mkopo huo mpya ni moja kati ya bidhaa ya kipekee nchini yenye lengo la kurahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wafanyakazi toka serikalini.

“Bidhaa yetu ya mkopo wa Executive, ni bidhaa itolewayo haraka, yenye ubunifu na rahisi katika upatikanaji wake na ya kipekee katika soko la Tanzania. Ni mkopo ambao utawawezesha wafanyakazi wengi toka serikalini kupata fedha na kuweza kuinua viwango vyao vya maisha kwa kujihusisha na miradi mikubwa mbali mbali.   Viwango vya mikopo hii ni kuanzia shilingi milioni kumi mpaka thelathini ambapo marejesho yake yananzia miezi sita mpaka miezi sitini,” alisema Moore. 

“Bidhaa ya mkopo ya ‘Executive’ ni bidhaa ya kipekee kwa soko la Tanzania, kutokana na kwamba mteja atakiwi kutoa dhamana yoyote ili kupatiwa mkopo. Inachukua masaa 48 tu kwa mteja kupatiwa fedha za mkopo,” aliongeza.

Naye Meneja Masoko wa Kanda wa FAIDIKA, Bw. Haule Stephen alisema kuwa muombaji anatakiwa kutoa stakabadhi mbili za mishahara ya miezi miwili iliyopita, taarifa ya kibenki ya akaunti kuanzia miezi miwili na kuendelea, Kitambulisho cha kazi na picha moja ya pasipoti, ili kujipatia mkopo huo. Na kuongeza kuwa viwango vya mikopo ya FAIDIKA vimekua kutoka kuanzia shilingi milioni kumi na kufikia shilingi milioni ishirini.  

“Dhumuni letu ni kuona viwango vya maisha vya watanzania vinakua kupitia upatikanaji rahisi wa huduma za kifedha,” alisema Bw. Stephen. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...