Afisa ustawi wa jamii na Maendeleo ya jamii jijini Arusha, Mwantumu Dossi
(kulia) akitembelea mradi wa shamba la mahindi unaoendeshwa na taasisi ya Gola Foundation jana katika kituo cha Kufikia watoto wa mitaani,katikati ni Mkurugenzi wa shirika hilo, Elisha Maghembe

Mkurugenzi wa shirika lisilokua la kiserikali la Gola Foundation, Elisha Maghembe amesema kuwa wameanza zoezi la kuwaondoa watoto wa
mitaani walioko jijini Arusha na kuwafikisha kwenye vituo maalumu vya
malezi lengo ikiwa ni kuwarudisha makwao pamoja na kuwapatia fursa ya
elimu waliyoikosa kwa muda mrefu.
Elisha alisema kuwa zoezi hilo limeanza mapema mwaka huu ambapo mpaka
sasa wamewakusanya watoto 25 na kuwapeleka katika kituo chao cha
malezi kilichopo wilaya ya Arumeru ambapo watoto watano walitambuliwa
na kuchukuliwa na wazazi wao.
Amesema kuwa watoto wa mitaani wanapokaa mtaani kwa muda mrefu
hujitumbukiza katika majanga ya matumizi ya madawa ya kulevya na
kufanya vitendo visivyofaa hivyo ameitaka jamii ishirikiane kutatua
tatizo hili ambalo ni janga kwa taifa.
“Tunapofika mtaani kuwaondoa watoto hawa wa mtaani tunakutana na
changamoto nyingi ikiwemo kukosa ushirikiano na watoto wenyewe na pia
wengine wanatumkishwa na ajira katika umri mdogo na baadhi ya watu
hivyo kufanya zoezi hilo kuwa gumu” Alisha Elisha
Afisa ustawi wa jamii na Maendeleo ya jamii jijini A Mwantumu Dossi
alifika katika kituo cha kufikia cha malezi ya watoto wa mtaani
kinachomilikiwa na Gola Foundation amesema kuwa Halmashauri ya jiji
itaangalia namna ya kushirikiana kutatua changamoto za watoto wa
mitaani.
“Tatizo la watoto wa mitaani ni tatizo sugu nimefika apa kujionea na
kama Jiji kuna mkakati Mahususi wa kuwaondoa watoto wa mitaani
utakaoanza 2015-2016” alisema Mwantumu
Mwenyekiti wa Baraza la watoto wilaya ya Arusha Hassan Omari alisema
kuwa juhudi za kuwaondoa watoto wa mitaani katika mazingira magumu na
hatarishi zinapaswa kuungwa mkono na kila mtu pamoja na serikali kwani
watoto ni taifa linalotegemewa kesho.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...