Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akisalimiana na Aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa sasa Mkoa wa Tanga Alhaj Salum Chima muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya kumuaga Ndugu Chima na kumkaribisha Ndugu Smythies Pangisa (katikati) aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara sasa Mkoa wa Rukwa. Hafla hiyo ilifanyika tarehe 13 Juni 2015 katika ukumbi wa Kanyau Sumbawanga Mkoani Rukwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya hafla hiyo ambaye pia ni Meneja wa SIDO Mkoa wa Rukwa Ndugu Martin Chang'a akitoa salam za utangulizi katika hafla hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya akizungumza katika hafla hiyo. Aliwaasa watumishi kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na ubunifu mkubwa na kwamba ndiyo siri pekee ya mafanikio katika utendaji wao wa kazi. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...