Na Bashir Yakub.
Wakati mwingine waliokopa kwa kutumia viwanja /nyumba huwa na mahitaji ya kuviuza. Wasiwasi wao mkubwa huwa ni kwa mtoa mkopo iwapo akijua eneo lililowekwa dhamana limeuzwa . Pia wanunuzi wa maeneo ambayo yamewekwa dhamana nao wakati mwingine huwa na wasiwasi juu kununua maeneo kama hayo.
Nilwahi kueleza namna ya kununua ardhi iliyowekwa mkopo japo sicho ninachozungumza leo. Leo naeleza hadhi ya kisheria ( legal status) kwa watu wa aina tatu. Kwanza sheria inasemaje kwa aliyechukua mkopo na kuweka dhamana nyumba/kiwanja na sasa anataka kuuza eneo hilo japo hajamaliza mkopo. Pili sheria inasemaje kwa mtoa mkopo ambaye anagundua kuwa eneo alilopewa kama dhamana na akatoa hela limeuzwa bila kupewa taarifa. Tatu Sheria inasemaje kwa huyu aliyeuziwa eneo lenye mkopo.
1.KUUZA NYUMBA/KIWANJA CHA DHAMANA.
Kwanza ieleweke vyema kuwa si dhambi hata kidogo kuuza eneo uliloweka dhamana ikiwa hilo litafanyika kwa kuzingatia misingi maalum ya kisheria. Kifungu cha 68 cha Sheria ya Ardhi kimezungumzia habari hii kwa namna fulani. Kubwa zaidi unapokuwa unaamua kuuza eneo uliloweka dhamana wakati ukijua hujamaliza deni ni kuhakikisha haufanyi hivyo kwa hila. Uza lakini isiwe kwa hila.
Kuuza kwa hila kwa maana hii hapa ni kuuza ambako kunalenga kukwepa kutolipa deni.Haya yanatokea sana, mtu anajua ana deni na eneo lake litauzwa muda wowote basi anaamua kuuza akiamini kuwa yule anayenunua atajuana na watu wa mkopo kwakuwa yeye atakuwa amekimbia au vinginevyo. Huku ndiko kuuza kwa hila. Aidha sheria imeeleza kuuza kutokuwa kwa hila ambako ni kuuza kwa kumshirikisha mtoa mkopo. Inatakiwa mtoa mkopo awe amearifiwa na akijua kila hatua ya kinachoendelea. Hii ni kwasababu pia mwisho wa siku mtoa mkopo atatakiwa kukabidhi kwa mnunuzi nyaraka ya kununulia ardhi kwakuwa anakuwa nayo yeye ikilinda deni.
2. JINAI KWA KUUZA ENEO LA DHAMANA.
Wengi wanaouza maeneo waliyoyaweka dhamana bila kutoa taarifa kwa watoa mikopo huwa wanatenda jinai ya kughushi. Hii ni kwasababu unapomuuzia mtu ardhi ni lazima umpatie nyaraka iwe hati, leseni ya makazi, ofa au hata mkataba wa kununulia ( sale agreement).
Na ikiwa mtu amechukua mkopo na hajamaliza kulipa basi nyaraka hii huendelea kuwa mikononi mwa mtoa mkopo. Kutokana na hilo ina maana mtu huyu akiuza atakuwa hana nyaraka yoyote na akiwa nayo basi ni ya kughushi . Mara nyingi haya hujitokeza maeneo ambayo hayana hati wala leseni za makazi ambapo huwa rahisi kwa mtu kuandaa mkataba wa kununulia na kumkabidhi mnunuzi kwa hadaa kuwa ndio alionunulia. Hii ni jinai kubwa sana ambayo huadhibiwa vikali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...