Kitambi ni ile hali ya tumbo kuwa kubwa na kuchomoza kwa mbele na wakati mwingine kufikia hatua ya kuniníginia.

JINSI KITAMBI KINAVYO PATIKANA

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kitaalamu, mwili wa binadamu una seli kati ya bilioni 50 hadi 200 za mafuta zilizogawanyika katika sehemu mbalimbali za mwili wa binadamu.
Kwa wanawake seli hizo zipo sana katika maeneo ya matiti, kwenye nyonga, kiunoni na kwenye makalio.

Kwa upande wa wanaume seli hizo zinapatikana sana kwenye kifua, tumboni na kwenye makalio pia. Mafuta ya tumbo yanayofanya kitambi hukusanywa kwa njia kuu mbili:
i. Njia ya kwanza ni mafuta kutoka kwenye tishu zilizo chini ya ngozi
ii. Na njia ya pili ni kutoka kwenye ogani za ndani kama moyo, kongosho n.k

SABABU ZA KUPATA KITAMBI
Sababu kubwa ya kitambi ni kukosekana ulingano wa nguvu(kalori) katika mwili wa mwanadamu, hali inayo sababishwa na mtu kula vyakula vinavyotia nguvu sana kuliko jinsi anavyoweza kutumia na kutoa kama taka mwili.

VYAKULA VINAVYO CHANGIA KULETA KITAMBI
Vyakula vinavyochangia kuleta kitambi ni pamoja na :
i. Vyakula vyenye mafuta mengi kama vile nyama nyekundu (iwe ni ya kuchemsha, kukaanga au kuchoma), nyama ya kuku wa kizungu ( iwe ya kuchemsha, kukaanga ama kuchoma ), mafuta ya kupikia, (hasa yale yatokanayo na bidhaa za wanyama, kama siagi, na jibini), viazi ya kukaanga kwa mafuta (chips) pamoja na pizza.
ii. Vyakula vyenye wanga mwingi kama vile ugali wa mahindi, mihogo, wali, mkate mweupe.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 01, 2015

    Kama una zaidi ya miaka 35 muone afisa lishe akupatie ushauri wa lishe bora. Kama si hivyo punguza mafuta kwenye chakula unachokula na punguza sukari pia. Fanya mazoezi ya kukutoa jasho kwa nusu saa kila siku, kama ni kutembea ongeza spidi usitembee kivivu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 01, 2015

    Punguza pia chakula ukihakikisha kila mlo una protini mboga na matunda

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...