Kampuni ya Kitanzania inayomilikiwa na Bw. Twalib Lubangula imepata tenda kubwa nchini Zambia ya kukarabati viwanda vya Cement Ndola na sehemu nyingine nchini.
Ni jambo la kujivunia kuwa Kampuni inayomilikiwa na Mtanzania kwa asilimia 100 kupata tenda kubwa nchi za nje na kampuni hiyo inafanya vizuri sana.
Mhe. Grace J. E. Mujuma Balozi wa Tanzania nchini Zambia akipata maelezo kuhusu mafanikio ya Kampuni ya Pan African Refractory Services Co. Ltd ya Tanzania kutoka kwa mmiliki wa kampuni hiyo Bw. Twalib A. Lubangula baada ya kuutembelea Ubalozi jijini Lusaka kwa ajili ya kujitambulisha leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...