Kampuni ya matangazo ya FLAMETREE iliyojikita Africa mashariki sasa imezinduliwa upya na kupewa jina jipya la RIGHT HERE TANZANIA, mabadiliko haya yametokana na kuingia kwa mwekezaji mpya wa kimataifa ambaye ameonyesha nia ya dhati ya kuwekeza kwenye kampuni hii kufuatia utendaji mzuri aliouona kwenye kampuni hiyo na kuamua kuongeza nguvu zaidi katika kuinua utendaji, uwekezaji huu unatarajiwa kuongeza tija na muamko wa wafanyakazi na wateja wao. Kufuatia mabadiliko haya sasa kampuni ya RIGHT HERE itaweza kuhudumia wateja wake kwa viwango vya juu zaidi huku idadi ya wabunifu na vitendea kazi vikiongezwa.
RIGHT HERE imechaguliwa kuwa mwakilishi kwa Tanzania wa kampuni kubwa ya matan- gazo ya PUBLICIS ambayo ni moja kati ya makampuni makubwa manne duniani kama WPP, Interpublic na Omnicom.
Akizindua jina hilo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam mwekezaji huyo Bwana Gerald Govaerts amesema, “nia na madhumini ya uzinduzi huu ni kuitambulisha kampuni hii kwa upya kwa watanzania, licha ya kuwapo hapa nchini kwa zaidi ya miaka mitatu.
Gerald aliendelea kusema “soko la Tanzania kwa sasa linakua kwa kasi na sekta ya ushirikiano inazidi kukua kwa viwango vya juu, hivyo umuhimu wa kutangaza masoko na bidhaa zinazozalishwa ni mkubwa mno, kwa kufanya hivi tunatoa nafasi kwa makampuni mengine kutambua uwepo wetu hapa Tanzania na Afrika mashariki na wao kuweza kuzitambua kazi tunazozifanya.
”Kufuatia uwekezaji huu mpya na ubia kwa kampuni ya kimataifa, nia kubwa ni kukuza sekta ya masoko kwa Afrika mashariki huku tukifanya kazi kwenye viwango vya kimataifa. Tunayofuraha kubwa kwa uwekezaji huu kwani utaongeza tija kwa watanzania wenye vipaji.
Kampuni ya RIGHT HERE inatoa huduma mbalimbali kama kuandaa matangazo ya biashara kwa niaba ya wateja, kununua nafasi za matangazo kwenye vyomba vya habari,kuandaa mikakati ya jinsi ya kukuza bidhaa yako, kuwatangazia wateja bidhaa zao kwenye mitandao mbalimbali na kuwashauri hali halisi ya masoko na ushindani ilivyo duniani kwa sasa.
“Ni furaha kubwa kuitambulisha kwenu kampuni ya RIGHT HERE” alisema Bi Jenny Woodier, meneja mkuu wa RIGHT HERE Tanzania, huku tukijivunia timu yenye wafanyakazi bora na kazi nzuri ambazo tumeshazifanya mpaka sasa kwa wateja wetu,licha ya kuandaa kazi nzuri zilizoendana na soko la wateja wetu lakini pia tumeonekana kimataifa na kupata nafasi ya kuwa wawakilishi wa kampuni kubwa yenye nia ya kuwekeza hapa Tanzania kwa hapo baadaye. Ubia huu na kampuni ya Publicis Africa Group utakuwa na manufaa makubwa kwa wateja wetu na kutuwezesha sisi kama RIGHT HERE kupanua wigo wetu wa kufanya kazi kimataifa.
Dhamira yetu ni kuona ushindani wa matangazo ya bidhaa kwa Tanzania unakua na kufikia viwango vya kimataifa. Mpaka sasa tumeweza kushinda tuzo mbali mbali za kimataifa.
Bi Jenny aliendeela kusema “ Kama kampuni tumefanya kazi hapa Tanzania kwa miaka mitatu na makampuni ya ndani na nje ya Tanzania ikiwamo makampuni ya simu, benki, taasisi zisizo za kiserikali,kampuni za samani za ndani, kampuni za sola na nyingine nyingi. Kwa miaka hiyo michache ya kufanya kazi kwa bidii na kutambulika kimataifa,kampuni ya RIGHT HERE sasa inasababu ya kujivunia ujuzi wa kufanya kazi za wazawa huku tukizifanya kwa viwango vya kimataifa. Kama wadau wa matangazo tunaamini ubunifu bora unaleta ushindani katika soko na kuweza kuifikisha bidhaa kwenye viwango vya kimataifa.
KUHUSU KAMPUNI YA RIGHT HERE.
Jina la RIGHT HERE linatoa maana halisi ya jinsi sisi tunavyofanya kazi kwa kuangalia walengwa wanataka nini na kufahamu umuhimu wao, lakini pia kama unatafuta mdau mwenye ujuzi na mwenye viwango vya kimataifa, watanzania wenye ubunifu na wanaoendana na hali ya soko, suluhisho pekee ni “RIGHT HERE”
Mshauri mkuu wa kampuni ya RIGHT HERE TANZANIA, Gerard Govaeas akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari katika Ukumbi wa mikutano katika Hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha copywritter and Culture Asnath Heriel na Mkurugenzi Mkuu Jenny Woodier.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano wa kampuni ya RIGHT HERE TANZANIA mkutano uliofanyika katika hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam leo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...