Kampuni ya mafuta na gesi ya Swala (Tanzania) Plc ("swala" au "Kampuni") inayo furaha kutangaza kwamba imefikia makubaliano ya kugawana umiliki na Kampuni ya Tata Petrodyne Limited ("TPL"), kampuni ambayo ni sehemu ya Kampuni ya Kimataifa ya Tata sons Limited, ambapo TPL itakuwa ikifanya shughuli zake kwenye maeneo ya leseni ya Pangani na Kilosa-Kilombero nchini Tanzania. Hii itaiwezesha Kampuni ya swala kubaki kwenye maeneo yake ya leseni na ili kupata fedha kwa ajili ya shughuli za utafutaji hapo baadaye katika njia ambayo itapunguza hasara kwa wanahisa wake wa sasa.

Kampuni ya Tata Sons Limited ni Mratibu wa uendeshaji wa shughuli kubwa za makampuni ya Tata na kumiliki hisa zote muhimu kwenye makampuni haya, na kwa kawaida inajulikana kama kundi la Tata (Tata Group). Kundi la Tata lina mtaji wa soko wa takribani dola za Kimarekani bilioni 110 na inawakilisha zaidi ya asilimia 8 ya jumla ya mtaji wa soko katika soko la hisa la Bombay.

Katika sekta ya mafuta na gesi, makubaliano ya kugawiana umiliki ni makubaliano yaliyoingiwa kwa mmiliki wa leseni moja au zaidi (anayegawa umiliki huo) na kampuni nyingine ambayo inataka kupata asilimia ya umiliki wa leseni hiyo kwa ajili ya kutoa huduma (na 'kujimilikisha). Makubaliano ya kugawana umiliki yanatofautiana na shughuli za kawaida kati ya wakodishaji wawili wa mafuta na gesi, kwa sababu cha msingi kuzingatia ni utoaji wa huduma, badala ya ubadilishaji rahisi wa fedha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...