Katibu Mkuu wa CCM,Ndg Kinana akisisitiza jambo mbele ya Wananchi (hawapo pichani),kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika viwanja vya stendi ya mabasi mjini humo.
Umati wa wakazi wa Chato mjini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia kwenye uwanja wa stendi ya Zamani.Katibu Mkuu wa CCM aliwaambia wananchi hao kuwa Serikali inabidi ifute kodi kandamizi zinazowazuia wananchi kurahisisha maisha yao.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati akihutubia
wakazi wa Chato mjini ikiwa siku ya kwanza ya ziara ya Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mkoani Geita.
Umati wa wakazi wa Chato mjini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akihutubia kwenye uwanja wa stendi ya Zamani.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Mkuu wa wilaya ya Chato
Ndugu Rodrick Mpogole, viongozi wa CCM wilaya ya Chato pamoja na
mafundi wa Tanesco akishiriki kutandaza waya za umeme katika mradi wa
umeme vijijini REA katika kijiji cha Mkungo,wilayani Chato mkoani Geita.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo mafupi mara baada
ya kuwasha mtambo wa maji uliojengwa Chato Mlimani kama ishara ya
uzinduzi wa mradi wa maji utakaohudumia wakazi wa mji huo leo, wakati wa
ziara yake katika mkoa wa Geita .
Kinana
anaendelea na ziara hiyo ya kikazi mkoani humo baada ya kumaliza ziara
kama hiyo mkoani Kagera jana, Kinana anaendelea na ziara hiyo
yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka
2010 na kuhimiza uhai wa chama, kukosoa na kutatua matatizo mbalimbali
yanayowakabili wananchi kwa maisha na maendeleo yao kwa ujumla
akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki katika ujenzi wa nyumba
ya daktari katika kijiji cha Ihanga wilayani Chato.
PICHA NA MICHUZI JR-CHATO
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...