Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiswaga Ng'ombe kuingia kwenye josho katika kijiji cha Nyakwasi, Nyang'hwale mkoani Geita.Kinana aliwapongeza wana kikundi cha Songambele kwa kupambana na magonjwa ya mifugo kwa kujenga josho la kisasa,Pia Ndugu Kinana aliwaasa Vijana kufanya kazi kwa bidii n,a kuacha kukaa vijiweni kupiga sogakwani hakuna njia ya mkato ya maisha,badala yake ni kufanya kazi kwa bidii ikiwemo suala zima la kujiletea maendeleo kama vile kujishughulisha na ufugaji,ukulima ili kujikwamua na Maisha,Kinana akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye  yupo mkoani Geita akitokea mkoani Kagera katika ziara ya Kuimarisha uhai wa chama,kukagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2010-2015 pamoja na kusikiliza matatizo ya Wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinanaakiangalia baadhi ya miradi ya akina mama wajasiliamali wa Nyang'hwale.
Katib Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwasha mashine ya kukoboa na kusaga,ikiwa ni ishara ya kuzindua mradi huo wa akina mama Wajasiliamali,katika kijiji cha Nyamgogwa,wilaya ya Nyang'hwale mkoani Geita.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kharuma ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa ili nchi isonge mbele inabidi matumizi yasiyo ya lazima yapunguzwe na vijana kuamini kuwa maisha ni kuchapa kazi na si kukaa vijiweni,aliwataka wananchi hao kuchagua viongozi wenye moyo na watu.
Mbunge wa Jimbo la Nyang'hwale Mhe.Hussein Nassoro Amaliakihutubia wakazi wa Kharumwa kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliokusanya wananchi wengi kuliko kawaida. 
 Katibu wa Itikadi na Unezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kharumwa,wilaya ya Nyang'hwale na kuwaambia kuwa Kiongozi ni mtu mwenye moyo wa uvumilivu na usikivu, kiongozi wa siasa hapaswi kuwa na mashitaka ya kupiga watu.
 Kaimu Mkuu wa mkoa wa Geita ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Nyang'hwale akihutubia wananchi wa kaa ya Kharumwa waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa michezo wa Kharumwa ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akifurahia jambo na Mwaandishi wa habari wa Magazeti ya Serikali (Daily News & Habari Leo),Bwa.Pius Lugonzibwa katika kijiji cha  Nyijundu,Wilayani Nyang'hwale mkoani Geita,alipokwenda kushiriki ujenzi wa vyumba vya madarasa vya shule ya sekondari ya Nyijundu.

PICHA NA MICHUZI JR-NYANG'HWALE,GEITA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...