Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana, akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Mpira, mjini Muleba mkoani Kagera.Ndugu Kinana yuko katika ziara ya siku kumi mkoani Kagera ya kuimarisha na kukagua utekelezwaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2010,ikiwemo pia kusikiliza matatizo ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Mpira wa Muleba mjini mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akiwa pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiwasalimia wananchi (hawapo pichani),walipokuwa wakiwasili kwa boti katika kisiwa cha Iroba-Bumbile,wilayani Muleba.

Safi.Nilitegemea wangeenda na CHOPPER lakini wakaenda na Mtumbwi wa kawaida,ni mfano wa kuigwa!.Na hivyo visiwa vingine ni vipi?Bumbile ni kisiwa kinajitegemea,Iroba ni kisiwa kinajitegemea.Kuna visiwa vingi hapo Muleba ()Galinzira,Ikuza,Kitua,Runeke,Mazinga,Majeje,Goziba,Maheiga,nk).
ReplyDeleteDavid V
Tazania kubwa unaenda kwa boti kwa barabara kweli tumejaliwa raslimali ardhi.
ReplyDelete