Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia Mkutano wa hadhara leo,
kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Bukoba, akiwa katika ziara ya kukagua
uhai wa Chama na ilani ya Uchaguzi ya CCM.Ndugu Kinana yuko mkoani Kagera kwa ziara ya siku kumi akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na baadhi ya maofisa wa chama hicho
Mbunge wa Bukoba mjini Hamis Kagasheki (kushoto) akihutubia wananchi
katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye viwanja vya Mashujaa
mjini Bukoba mkoani Kagera.
Wananchi wa mji wa Bukoba mjini na wafuasi wa chama cha CCM wakishangilia jambo wakati Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pichani katikati alipokuwa akizungumza
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia mkutano wa
hadhara katika viwanja vya Mashujaa mjini Bukoba leo, akiwa katika ziara
ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana mkoani Kagera.
Mkuu
wa Mkoa wa Kagera,Mh.John Mongella akiwasalimia Wananchi na
Wanachama wapenzi wa CCM,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya
leo katika uwanja wa Mashujaa,mkoani Kagera.
PICHA NA MICHUZI JR-BUKOBA
Haya mambo ya kupanda meza hatari, tengenezeni majukwaa imara viogozi wayaatumie.
ReplyDelete