Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Peter Malebo Mjumbe wa Kamati ya Mgusu Miners Co. Oparative Society Limited jinsi mchanga unavyosafishwa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndug Kinana leo amehitimisha ziara yake ndani ya mkoa wa Geita kwa kutembea kilometa 1680 kwa Gari,ametembelea Majimbo sita na Wilaya zake sita,huku akiwa amehutubia mikutano 78,mikutano 72 ya hadhara na mikutano 6 ya ndania.Ndugu Kinana ametembelea miradi 53 ya Maendeleo,miradi mitano ya CCM.Kama vile haitoshi Ndgu Kinana amejizolea Wanachama wapya 6816,Wapinzani wakiwa 640 hasa kutoka CHADEMA.
Ndugu Kinana akiwa na msafara wake kesho anaanza ziara Mkoani Mwanza ya Kuimarisha uhai wa chama,kuhimiza na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2010-15,sambamba na kusikiliza matatizo ya Wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.
Baadhi
ya Wachimbaji wadogo wadogo wakiendelea na shughuli zao za kusaka
Dhahabu katika eneo waliloachiwa wachimbaji hao eneo la Mgusu,wilayani
Geita mkoani Geita.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyeshwa dhahabu ambayo tayari imeshapatikana baada ya kupitia hatua zote hizo kutoka kwa Mjumbe wa Bodi ya Mgusu Miners Co Oparative Society Limited Bw.Abdul Jumbe.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mbunge wa viti maalum mkoa wa
Geita Mh. Vick Kamata wakinyanyua mikono juu wakati wakikabidhi baiskeli
za viongozi wa kata wa Umoja wa wanawake Tanzania (UWT) zilizonunuliwa
na Mbunge huyo, katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa
Nyankumbu.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi katika
Uwanja wa Shule ya Msingi, Nyankumbu, katika Kata ya Kalangalala, akiwa
katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama
mkoani Geita leo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Kinana akipokea baadhi ya wafuasi wa chama cha
CHADEMA,waliokuwa wakirudisha kadi na kujiunga na chama cha CCM,kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa
Nyakumbu,mkoani Geita.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha wachimbaji dhahabu wadogo wadogo,Mkoani Geita.
PICHA NA MICHUZI JR-GEITA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...