Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara katika Mji Mdogo wa Katoro, wakati wa ziara Jimbo la Busanda, wilayani Geita, Mkoa wa Geita, ambapo aliwaahidi wachimbaji wadogo wadogo kulitafutia ufumbuzi wa kuwapatia vitalu vya machimbo eneo la Nyarugusu linalomilikiwa na Stamico, wilayani Geita.

Ndugu Kinana ambaye ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, yupo mkoani Geita kwa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, pamoja na kupokea kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi. eneo la Nyarugusu. 
  Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Katoro waliojitokeza kwa wingi ,Katika mkutano huo Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi aliwaambia wakazi hao vyama vingi vya siasa vimeshindwa kuendelea kutokana na kukosa sera,kushindwa kusimamia mambo pamoja na kuwa na viongozi wasiokubali mabadiliko na kung'ang'ania madaraka.
Wakazi wa Katoro waliojitokeza kwa wingi ,Katika mkutano huo Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi aliwaambia wakazi hao vyama vingi vya siasa vimeshindwa kuendelea kutokana na kukosa sera,kushindwa kusimamia mambo pamoja na kuwa na viongozi wasiokubali mabadiliko na kung'ang'ania madaraka.
  Sehemu ya umati wa watu waliofurika katika mkutano wa hdhara uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Kinana katika Mji Mdogo wa Katoro, Jimbo la Busanda, mkoani Geita leo.


Mbunge wa Jimbo la Busanda Mhe.Mh Lolensia Bukwimba akihutubia wakazi wa Katoro kwenye mkutano wa hadhara ambao mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
PICHA NA MICHUZI JR-BUSANDA,GEITA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...