Wananchi wa kijii cha Rukoma kata ya Rukoma wakiwa wamekusanyika wakimsilikiza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa hadhara jioni ya leo Bukoba vijijini.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia Wananchi wa kijiji cha Katoro jioni ya leo wilayani Bukoba vijijini,mkoani Kagera.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akiwahutubia Wananchi wa kijiji cha Katoro jioni ya leo wilayani Bukoba Vijijini,mkoani Kagera.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kushoto , Mbunge wa jimbo la Bukoba Vijijini Mh. Jason Rweikiza katikati  na  Novatus Nkwama Mwenyekiti wa CCM  Bukoba Vijijini wakishiriki kufukia mabomba katika mradi wa maji unaotekelezwa na serikali  katika kata ya Ibyera Bukoba vijijini wakati Katibu Mkuu huyo akiendelea na ziara yake katika jimbo hilo leo.

 Katibu Mkuu huyo yuko katika ziara ya kikazi  katika mikoa ya Kagera , Geita na Mwanza akikagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 huku akihimiza uhai wa Chama akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akitoka ndani ya Ofisi ya CCM ya Kijiji cha Rukoma aliyoizindua leo,Bukoba Vijijini mkoani Kagera,kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na kushoto ni Mbunge wa Bukoba Vijijini Mh.Jason Rweikiza.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Ndugu John Mongella akizungumza na wananchi na kuwaeleza kuwa wasitishwe na mtu yeyote katika suala zima la kujiandikisa," asiwatishe mtu nendeni mkatumie haki yenu ya kikatiba mkajiandikishe katika daftari la wapiga kura katika kata ya Katoro Bukoba Vijijini na wala msiogope",alisema Mh.Mongella. 
 Mbunge wa jimbo la Bukoba Vijijini Mh Jason Rweikiza akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Katoro Bukoba Vijijini.
 Wananchi waliokusanyika katika mkutano wa hadhara katika uwanja wa Katoro wilayani Bukoba vijijini,mkoani Kagera jioni ya leo.

PICHA NA MICHUZI JR-BUKOBA VIJIJINI


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...