WAKAZI wa Mkoa wa Kigoma, wameiomba Kampuni ya Msama Promotions kuwapelekea uzinduzi wa albamu tatu za mwimbaji mahiri wa nyimbo za injili nchini Boniface Mwaitege.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama amepokea maombi mengi kwa wakazi wa mkoa huo wakihitaji uzinduzi huo ufanyike mkoani kwao.

“Nimepokea maombi ya wakazi wa Kigoma wakihitaji uzinduzi wa muimbaji nguli, Bonny Mwaitege ambaye anatarajia kuzindua albamu tatu,” alisema Msama.

Msama alisema mbali ya Kigoma mikoa mingine imeonesha nia ya kutaka uzinduzi huo ufanyike mikoani kwao. Alisema  wakazi wa Kigoma wanatamani kumuona akifanya onyesho mkoani humo kwa kuwa ni moja ya waimbaji ambao wamekuwa wakiwashuhudia wakifanya makubwa jukwaani.

Aidha Msama alisema kuwa kujitokeza kwa baadhi ya wananchi wa mikoa mbali hiyo kuomba, inampa moyo kuona watu wamemgeukia Mungu na kutaka kupata neno kutoka kwa waimbaji wa muziki wa injili ambako alisistiza kuwa  yuko pamoja nao na atajitahidi.

Mwimbaji huyu machachari ambaye anatamba na nyimbo mbalimbali kama Mama ni mama, Mke mwema, Wakusamehe, fungua moyo wako na njoo uombewe na Yesu yupo anatarajia kuzindua albamu hizo tatu Agosti 2 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Msama alisema kuwa Kamati ya Maandalizi itaketi na kujadili kwa sababu ni mikoa mingi iliyoomba kupelekewa uzinduzi huo hivyo ni jambo la kujipanga kuona namna itakavyoweza kufanya na kuwafikia katika mikoa yao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...