Dkt. Agnes Kijazi, Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (akiwakilisha Tanzania) katika picha ya pamoja
na washiriki wa kikosi kazi cha “African Ministerial
Conference on Meteorology (AMCOMET) Technical Task Force on African Regional
Space Programme on Meteorology” Geneva, Uswisi tarehe 10 juni 2015.
Tanzania ambayo ni
mwenyekiti wa kikosi kazi cha “African Ministerial Conference on Meteorology
(AMCOMET) Technical Task Force on African Regional Space Programme on
Meteorology” iliongoza kikao cha kikosi kazi hicho kilichofanyika tarehe 10
Juni 2015 sambamba na Mkutano Mkuu wa 17 wa Shrikika la Hali Duniani (WMO-CONGRESS-17)
huko Geneva nchini Uswisi. Kikao
kiliendeshwa chini ya Dkt. Agnes Kijazi kwa mafanikio makubwa.
Mkutano huo wa kikosi
kazi ulifanyika kwa kutumia fursa ya kuwepo washiriki katika Mkutano Mkuu wa 17
wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO Congress-17). Lengo la mkutano lilikuwa kubadilishana
uzoefu na nchi ambazo zimepiga hatua katika masuala ya hali ya hewa katika anga
za juu (Space Meteorology). Aidha kikao pia kilijadili upatikanaji wa vyanzo
vya mapato ambavyo vitasaidia kufanikisha programu hii na miradi itakayofanyika
wakati wa utekelezaji wa program hii.
Dkt.
Agnes Kijazi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania ambaye pia ni
mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO)
na mwenyekiti wa mkutano huo akiendesha Mkutano wa Kamati ya Kikosi Kazi cha
Programu ya anga za juu ya AMCOMET, Geneva, Uswisi. Kulia kwake ni Dkt. Joseph
Kanyanga kutoka Zambia akiwakilisha AMCOMET Bureau na Dkt. Amosi Makarau, Rais
wa RA1; Kushoto kwake ni wawakilishi wawili wa Sekretarieti ya Shirika la Hali
ya Hewa Duniani (WMO Secretariat).
IMETOLEWA NA: MONICA MUTONI-AFISA MAHUSIANO TMA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...