Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akizungumza na Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro leo Juni 18, 2015, wakati shukrani kwa udhamini wa kishindo alioupata kutoka wa WanaCCM hao, ili aweze kupata ridhaa ya Chama chake katika kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 33,780. Picha Othman Michuzi.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za wanachama 33,780 wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, waliomdhani ili aweze kupata ridhaa ya Chama chake katika kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Anaekabidhi fomu hizo ni Katibu wa CCM Wilaya ya Moshi Mjini, Loth Ole Nesele.
Mh. Lowassa akiwasalimia wananchi wa Mji wa Muheza sambamba na kuwatakia Heri ya Mfungo Mtukufu wa Mwezi wa Ramadhani, wakati akiwa safarini kuelekea Mkoani Kilimanjaro kusaka wadhamini watakamuwezesha kupata ridhaa ya CCM kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Juni 18, 2015.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Edward Lowassa alipata wasaa wa kwenda kuhani msiba wa Baba Mzazi wa Balozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe, Mh. Adadi Rajab, Marehemu Mzee Rajab nyumbani kwao Muheza, Mkoani Tanga. anaezungumza na Mh. Lowassa ni Mama Mzazi wa Mh. Adadi Rajab, Bi. Fatuma Omar.
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mh. Steven Ngonyani "Prof. Maji Marefu" (katikati) pamoja na wananchi wa Korogwe wakiwa wamefunga barabara kuuzuia msafara wa Mh. Lowassa ili aweze kuzungumza nao, huku wakimuuga mkono katika safari ya Matumaini.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...