Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua rasmi Chanjo ya  watoto kuzuia maambukizi ya magonjwa katika kata ya Nyakisasa kijiji cha Kashinga akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani Ngara mkoani Kagera,lengo la ziara hiyo likiwani ni kukagua utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010 na kuhimiza uhai wa chama, Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na ktibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na viongozi mbalimbali wa CCM  kutoka mkoa wa Kagera.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi mbalimbali za waliokuwa wanachama wa Chama cha CHADEMA mara baada ya kurejesha kwake na kujiunga na CCM katika mji wa Rulenge.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ngara Mama Constansia Buhie wakizikusanya kadi  mbalimbali za wafuasi wa upinzani na kuzikabidhi kwa viongozi hao wa CCM,ikiwa ni ishara ya kujiunga na chama hicho cha CCM
 Baadhi ya kadi zilizorejeshwa kwa Kinana na wananchi hao na kujiunga na CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na mhandisi wa kampuni ya kichina ya TKPE Bw.Ton Minyang wakati alipokagua ujenzi wa  Mtambo wa umeme  vijijini REA unaojengwa katika kijiji cha Djuruligwa kata ya Kabanga wilayani Ngara.
 Wananchi wa Ngara mjini wakishangilia jambo katika mkutano wa hadhara wa CCM
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Abdulrhaman Kinana akiwahutubia wananchi wa Ngara mjini,Kinana ameitaka Serikali kurahisisha utoaji wa leseni kwa wafanyabiashara , madereva wa magari na bodaboda badala ya kuacha watu wanasumbuka kutafuta leseni umbali mrefu tena kwa gharama kubwa.

Kinana amesema kuwa  moja ya ombi la wananchi hao ilikuwa ni kuomba kurahisishiwa kupata leseni ili kuondoa usumbufu wanaoupata sasa.Alisema Serikali lazima iweke mazingira mazuri ya kutoa leseni kwa wananchi wakiwamo wafanyabishara na madereva bodaboda huku akieleza hakuna sababu ya kutumia gharama kubwa kwa ajili ya leseni. 

 KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa mji wa Ngara Mjini kwenye mkutano wa hadara,Nape Nnauye alisema kuwa hakuna sababu ya Watanzania kuingia kwenye mpasuko kwa sababu ya mchakato wa katiba mpya na kuashauri ni vema mjadala ukafungwa kwenye nyumba za ibada. Amesema inasikitisha unapoona baadhi ya viongozi wa dini badala ya kuhubiri neno la Mungu na kuwaunganisha Watanzania wanatumia nafasi yao kuwagawa wananchi kwa sabababu ya Katiba mpya.

PICHA NA MICHUZI JR-NGARA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...