Hatimaye siku imewadia, tarehe
iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa taarab wa jiji la Mwanza
ndio hii hapa - ni Mzee Yussuf na Isha Mashauzi katika onyesho la kukata na shoka
ndani ya Villa Park leo usiku.
Ni onyesho linalokutanisha
miamba miwili ya taarab ambapo licha ya kuchukuliwa kama mtu na mwanae lakini
upinzani mkubwa unatarajiwa kutawala katika onyesho hilo lililopewa jina la
usiku wa baba na mwana.
Wasanii wote wawili (Isha na
Mzee) wameahidi kumimina uhondo wa aina yake Alhamisi ya leo hapo Villa Park -
Mwanza huku kila mmoja akikataa kuanika silaha (nyimbo) zake za maangamizi.
Hii ni mara ya kwanza kwa Mzee
Yussuf na Isha Mashauzi kukutana jukwaa moja nje ya Dar es Salaam tangu Isha
alipojiengua Jahazi Modern Taarab ya Mzee Yussuf zaidi ya miaka minne
iliyopita.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...