Umati wa WanaCCM pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Iringa, ukiwa umefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Samora Mkoani humo, kumpokea Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa, wakati akiwasili kwenye Uwanja huo tayari kwa kukabidhiwa fomu za WanaCCM waliomdhamini ili kumuwezesha kupata ridhaa ya Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Iringa wamevunja rekodi ya Mbeya kwa uwingi wa wanachama waliomdhamini Mh. Lowassa, amepata wadhamini 58,562 kwa mkoa wa Iringa pekee na ukiongeza na wanaCCM 10,900 wa mkoa wa Njombe alikopita pia kupata udhamini, unafanya jumla kuu ya wadhamini wote kufikia 69,462.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Iringa wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Samora Mkoani Iringa, tayari kwa kukabidhiwa fomu za WanaCCM waliomdhamini ili kumuwezesha kupata ridhaa ya Chama chake kuwania Urais kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Chifu wa Wahehe wa Mkoani Iringa, Chifu Hassan Adam Sapi akizungumza machache na kutoa baraka za kichifu kwa Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa katika Safari yake ya Matumaini.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Iringa, Dk. Owdenburg Mdegela akisoma Neno kutoka kwenye simu yake.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Marafiki zake ambao ni Wakazi wa Mji wa Makambako, Alfred Mtweve (kulia) na Angelusi Muhingu wakati aliposimama kuwasalimia WanaCCM na Wananchi wa Mji huo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipokea fomu za WanaCCM zaidi ya elfu 10 wa Mkoa wa Njombe waliomdhamini kutoka kwa Katibu wa CCM wa Wilaya ya Njombe, Clemence Mponzi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...