VIONGOZI wa dini wakiwemo Maaskofu na Wachungaji wa Makanisa mbalimbali hapa nchini wamebariki uzinduzi wa albamu tatu za mwimbaji mahiri wa muziki wa Injili hapa nchini Bonny Mwaitege, unaotarajia kufanyika Agosti 2 kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama sababu za viongozi hao wa dini kutoa baraka kwa albamu hizo ni kutokana na umahiri wa muimbaji huyo.
Msama alisema amepokea baraka hizo kutoka kwa viongozi hao wa dini kwa sababu uzinduzi huo unashirikisha albamu tatu kwa pamoja, jambo ambalo linaonesha ni ukomavu na umahiri katika kufanikisha neno la Mungu ipasavyo.
“Uzinduzi wa Bonny Mwaitege utakuwa ni wa aina yake kwa sababu viongozi wa dini mbalimbali wametia baraka kwa maneno matakatifu ambayo yatafanikisha ufikishwaji wa neno la Mungu kwa jamii ipasavyo,” alisema Msama.
Msama alisema baraka hizo za viongozi wa dini zinakwenda sambamba na maombi ya kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 25 mwaka huu hapa nchini ambao utahusu urais, Wabunge na Madiwani.
“Viongozi wa dini ndio wanafanikisha tunu ya amani tuliyonayo, hivyo wameongeza chachu ya maombi ya amani hiyo tuliyoachiwa na baba wa Taifa, Mwalim Julius Kambarage Nyerere,” alisema Msama.
Aidha Msama alisema hivi sasa wanaendelea na maandalizi ya kurekodi albamu hizo jijini Mwanza ili kupata ladha nzuri ya nyimbo hizo za kumuimbia na kumtukuza Mungu.
“Waandaaji wanaendelea na kazi yao ya kufanikisha kurekodi albamu hizo ambazo zitakuwa na ubora wa aina yake kwa sababu umahiri wa watendaji wake ambao ni wa kampuni yake ya Video Productions. Msama alitoa wito kwa mashabiki wa muziki wa Injili kujiandaa kupata kazi bora ya muimbaji huyo ambaye anashika anga la muziki huo Afrika Mashariki na Kati.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...