Balozi wa Tanzania nchini Malaysia Dkt. Aziz Ponary Mlima aliwaalika Mabalozi wa nchi mbali mbali kuja kutembelea Tanzania hivi karibuni.
Mabalozi hao kutoka Kuala Lumpur Malaysia walitembelea mbuga za wanayama za Serengeti, Ngorongoro na walifanya ziara mjini Zanzibar.
Mabalozi hao ni Waheshimiwa Viorica na Constantin Nistor (Romania), Stephen Mubiru (Uganda), Dkt. Aziz Ponary Mlima(Tanzania), Isabela Mhlanga( Afrika Kusini), na Bwana Rogatius Shao (Naibu Balozi-Tanzania).
Mabalozi walipowasili Kibo Palace Hotel, Arusha na kupokelewa na Naibu Waziri wa Maliasili.na Utalii Mheshimiwa Mahmud Mgimwa, Bwana Alan Kijazi Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA na Bwana Pascal Shelutete Meneja wa Mawasiliano na Masoko wa TANAPA.
Sehemu ya wanyama katika Mbuga ya Serengeti, wakati walipotembelea hifadhi hiyo.
Wakiwa kwenye uwanja wa Ndege wa JK Nyerere Walikutana na Mabalozi wengine ambao ni Balozi Thami Mseleku Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania na Balozi Chabaka Kilumanga na Mkewe walipokutana VIP Lounge kabla ya kuondoka na kurejea Kuala Lumpur.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...