Baadhi ya Wadau wa Mahakama kutoka Magereza,Ofisi ya DPP, Polisi  wakiwa katika Mkutano wa Majaji wa Mahakama ya Rufani unaolenga katika kupata maoni ya wadau juu ya njia zitakazowezesha kusaidia kumaliza mashauri/rufani zinazoletwa Mahakama ya Rufani kwa wakati.
Baadhi ya Wahe. Majaji, Maafisa wa Mahakama pamoja na Wadau wa Mahakama wakiwa katika Mkutano katika majadiliano juu ya Maboresho ya umalizaji wa Mahakama katika ngazi ya Mahakama ya Rufani (T) Kwa muda mrefu Mahakama ya Tanzania imekuwa katika jitihada mbalimbali za kushirikishana wadau mbalimbali pamoja na njia nyinginezo zote zikiwa zinalenga katika kuboresha huduma ya utoaji haki katika ngazi mbalimbali za Mahakama I.e. Kuanzia Mahakama ya Rufani hadi katika ngazi ya Mahakama ya Mwanzo nchini. 
 Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kikao (katikati), Mhe. Edward Rutakangwa, Jaji wa Mahakama ya Rufani (wa pili kushoto), Mhe. Engela Kileo, Jaji wa Mahakama ya Rufani (wa kwanza kushoto), Mhe. Nathalia Kimaro, Jaji wa Mahakama (wa kwanza kulia), Mhe. Shaaban A. Lila, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania (wa pili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na Wahe. Majaji wengine wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu Mara baada ya kufungua rasmi Mkutano wa Majaji wa Mahakama ya Rufani unaolenga katika kupata maoni ya wadau juu ya njia zitakazowezesha kusaidia kumaliza mashauri/rufani zinazoletwa Mahakama ya Rufani kwa wakati.
 Meza Kuu ikiwa katika picha ya pamoja na Wasaidizi wa Sheria wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu na Maafisa wengine wa Mahakama walioshiriki katika Mkutano huo.
Meza Kuu ikiwa katika picha ya pamoja na Maafisa mbalimbali wa Mahakama ya Tanzania Katika Hoteli ya Oceanic View iliyopo Bagamoyo. 
Picha na Mary Gwera, Mahakama

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...