Baadhi ya wananchi waliotembelea katika banda la Mahakama ya Tanzania lililopo katika maonesho ya Utumishi wa umma yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam wakipata maelezo/ufafanuzi kutoka kwa Afisa wa Mahakama juu ya taratibu mbalimbali za kimahakama.
 Wananchi wakipata maelezo/ufafanuzi kutoka kwa Afisa wa Mahakama juu ya taratibu mbalimbali za kimahakama.
 1.   Mhe. Hussein Kattanga (aliyesimama ndani ya banda katikati), Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Mhe. John Kahyoza, Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania (wa kwanza kushoto, ndani ya banda) na Mhe. Warsha Ngh’umbu, Mkurugenzi Msaidizi wa Ukaguzi, Mahakama ya Tanzania (wa kwanza kulia) wakibadilishana mawazo na baadhi ya wananchi waliotembelea katika banda la Mahakama ya Tanzania lililopo katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika Viwanja vya Mnazi Mmoja. Mahakama ni moja ya Taasisi iliyoshiriki katika Maonesho hayo muhimu lengo likiwa ni kutoa elimu kwa wananchi na pia kutoa nafasi kwa wananchi kutoa malalamiko yako pamoja na maoni katika uboreshaji wa utoaji huduma za Mahakama.

1.   Mhe. Hussein Kattanga, Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa Wizara ya Katiba na Sheria alipotembelea katika banda lao. Maonesho haya ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanatarajiwa kumalizika rasmi tarehe. 23.06.2015. Picha na Mahakama

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...