Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Mvomero, Amos Makalla amekabidhi pikipiki tano kwa kata mpya tano za Chama cha Mapinduzi (CCM) ili kuwasaudia watendaji na viongozi wa Chama kufanya kazi za Chama kwa wepesi na ufanisi.

Akikambidhi pikipiki hizo, Mbunge wa Mvomero alimueleza mwenyekiti wa wilaya ya Mvomero ndg Abdalah Mtiga kuwa msaada huo ni muendelezo wa kukisaidia Chama wilaya ya Mvomero kwani awali alisaidia pikipiki 23 na hizo 5 inafanya jumla ya pikipiki alizosaidia Chama kuwa 28 zenye thamani ya sh 56,000,000.

Akipokea msaada huo mwenyekiti wa wilaya hiyo, ndugu Abdalah Mtiga alimshukuru sana mbunge huyo kwa Moyo wake wa kukipenda Chama kwani ni wabunge wachache sana wenye Moyo kama wa mbunge Amos Makalla. Aliwataka watendaji kutunza pikipiki hizo na zitumike kwa shughuli za chama na si vinginevyo.
Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Mvomero, Amos Makalla akiongea katika hafla ya kukabidhi.
Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Mvomero, Amos Makalla  akimkabidhi pikipiki hizo, mwenyekiti wa wilaya ya Mvomero, Ndg. Abdalah Mtiga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...