Mkurugenzi
wa Upelelezi wa makosa ya Jinai,(CP) Diwani Athuman akizungumza na
waandishi wa habari hawapo pichani leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Wizara ya mambo ya Ndani juu ya Operesheni usalama
imetokana na maamuzi yaliyofikiwa kwenye mikutano ya Wakuu wa Majeshi
ya Polisi kati ya Nchi za Kusini mwa Afrika na Mashariki mwa Afrika
waliokutana chini ya mwavuli wa (SARPCCO) na (EAPCCO) uliofanyika
Johanesburg nchini Afrika Kusini.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Upelelezi wa
Makosa ya Jinai CP, Diwani Athumania leo katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya mambo ya ndani jijini Dra es Salaam.
(
Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Mkutano
wa maandalizi kwa ajili ya Operesheni hii ulifanyika kule
Pretoria Afrika Kusini mnamo tarehe 23-24 April,2015. Wajumbe
walikubaliana kufanya Operesheni ya pamoja na kwa wakati mmoja Mkutano
huo uliamua pia kuwa makosa yafuatayo yapewe kipaumbele, Wizi wa magari, Madawa ya kulevya, Silaha haramu na milipuko, Wahamiaji haramu na biashara
haramu ya binadam, Ugaidi , Biashara haramu ya madini, Wizi wa Miundombinu
ya Umeme na Nyara za Serikali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...