Mwenyekiti wa klabu ya Gymkhana Dioniz Malinzi akipiga mpira
wakati wa ufunguzi wa mchezo wa gofu kwa ajili ya kuchangia ujenzi
wa maktaba na vifaa vya kompyuta vya Shule ya Sekondari ya Mtakuja.
Na Beatrice Lyimo- Maelezo
Bahari Rotary Klabu ikishirikiana na HANSA GROUP wamefanya harambee ya
tano kwa ajili ya kuchangia Shule ya Sekondari Mtakuja iliyopo Kunduchi jijini
Dar es Salaam.
Harambee hiyo iliyofanyika katika Viwanja vya Gymkhana kwa kuwa shindanisha
washiriki kucheza mchezo wa Gofu kwa lengo la kukusanya kiasi cha Shilingi
Milioni 40 za kitanzania kwa ajili ya kutatua changamoto zinazoikabili shule hiyo
ikiwemo Maktaba ya shule na Maabara.
Akizungumza na waandishi wa habari Rais wa Klabu hiyo Bw. Ally Abdallah
alisema kuwa Shule ya Sekondari Mtakuja ina wanafunzi 1,141 na inakabiliwa na
ukosefu wa Maabara ya mafunzo kwa vitendo, vitendea kazi, viti, meza, pamoja na
madawati.
“Tumeona changamoto nyingi zinazoikabili shule hiyo na jamii inayowazunguka
hivyo tumejitolea kukabiliana nazo kwani dhima ya Bahari Rotary Club ni
kubadilisha jamii kwa ujumla haswa kwa changamoto zinazojitokeza kwa
wanafunzi,”
“Mwaka huu tumejitoa kwa ajili ya Shule ya Sekondari Mtakuja ili
kuwatengenezea mazingira mazuri ya kusoma kwani watoto hawa ni Viongozi wa
kesho hivyo ni wajibu wetu kuwaanda” aliongeza Bw. Abdallah.
Awali Bahari Rotary Club ilichangisha kiasi cha shilingi Milioni 20 za kitanzania
kwa ajili ya ukarabati wa shule hiyo ikiwemo Uzio wa ukuta na Geti, kununua
Matanki ya Maji na kuimarisha mfumo mzima wa usambazaji wa maji shuleni
hapo aliongeza Bw. Abdallah
Kwa upande wa Meneja Masoko wa HANSA GROUP Bw. Reuben Richard
alifafanua kuwa Bahari Rotary Club imefanikiwa kusambaza maji safi na salama
katika shule tofauti jijini Dar es salaam na kugundua kuwa shule nyingi jijini
zinauhitaji maji safi na salama.
Fuchs Oil, Eco bank, Hansa Group, Oryx Oil, Tanzania Distilleries LTD, Satuguru
Travel, Car and General, R.K. Chudasama, NAS Tyres Services Ltd, Tecnowares,
Scania Tanzania Limited, Spice Net, Oilcom, Minex Logistics, Bank of India and
SBS (T) Ltd ni baadhi wa wadhamini waliojitokeza kudhamini mashindano hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...