Miss Universe Tanzania 2014 Caroline Bernard leo amekabidhi
msaada pamoja na kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa watoto wa kike katika shule ya msingi
Msimbazi Mseto jijini Dar es salaam, ukiwa ni mwendelezo wake katika kufanya kazi za kijamii.
Caroline ambaye ndiye aliyetwaa
taji la Miss Universe Tanzania 2014 ataendelea kulitumikia taji lake kama mrembo mtawazwa
ingawa alishindwa kwenda kushindana kimataifa kutokana na sababu za kiafya.
Caroline alishindwa kwenda kushiriki kwenye mashindano ya kimataifa2014 na badala yake
kwenda mshindi wa pili Nale Boniface mara baada ya kuumia kidole cha mguu wiki chache
kabla ya mashindano.
Mpaka atakapokabidhi taji baaadae mwaka huu, Caroline ataendelea
na taji lake na ndiye atakayemvisha mtaji mshindi wa 2015.
Msaada alioutoa caroline ni pamoja na vitaulo vya kinamama (hygiene pads) vya kujihifadhia
wakati wa hedhi na karatasi ya kujisafishia maarufu kama tissue.
“Nimelenga kushughulika na watoto wa kike hasa wa shule ya msingi darasa la sita na la saba
kwani hawa ndio wanaotakiwa kujitambua zaidi hususani mabadiliko yao ya kimwili huanzia
hapa.”Alisema mrembo Caroline.
Miss Universe Tanzania ilianza mashindano yake mwaka 2007 na mshindi wake alikuwa
Mwanamitindo Flaviana Matata na aliweza kuitoa kimasomaso nchi yetu ya Tanzania kwa
kushika nafasi ya Sita kidunia.
Mwaka uliofuata, 2008 mrembo Amanda Ole Sululu alimrithi
Flaviana Matata na kuvaa taji la Miss Universe Tanzania 2008 akifuatiwa na mrembo Illuminata
James mwaka 2009, kisha Hellen Dausen mwaka 2010.
Baadae taji lilichukuliwa na Nelly
Kamwelu 2011 na mwaka jana 2012 taji lilinyakuliwa na mrembo Winfrida Dominic. Mwaka
2013 taji lilienda kwa mrembo Betty Boniface na hatimaye kumuachia mikoba mrembo Caroline
Bernard Miss Universe 2014.
Miss Universe Tanzania 2014 Caroline Bernard akitoa elimu ya afya ya uzazi kwa watoto wa kike katika shule ya msingi Msimbazi Mseto Dar es salam
Caroline akitoa misaada ikiwa ni pamoja na vitaulo vya kinamama (hygiene pads) vya kujihifadhia wakati wa hedhi na karatasi ya kujisafishia maarufu kama tissue.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...