Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa,Ndugu Allan Kijazi akizungumza jambo,wakati
wa ufunguzi wa Warsha ya Wahariri wa Habari Tanzania,mapema leo asubuhi jijini
Mwanza.Ndugu Kijazi alisema kuwa Utalii ni sekta mtambuka na inachochea ukuaji
wa sekta nyingine ikiwa ni pamoja na kilimo, usafirishaji wa anga na barabara,
huduma za fedha, huduma za chakula na malazi kudorora kwa sekta nyinginezo.
Katika
ufunguzi wa Warsha hiyo,Ndugu Kijazi alisema kuwa, Kauli
mbiu ya Mkutano wa mwaka huu ni “Wajibu wa Vyombo vya Habari katika
kukuza utalii”,aliongeza kusema kuwa pamoja na kuelezea shughuli za TANAPA,
mada zitakazowasilishwa zitahusu masuala ya Utalii na Uhifadhi na namna
wanahabari wanavyoweza kushirikiana na TANAPA katika kuhimiza uhifadhi na
kuendeleza utalii.
"Mada kuu
nne zitawasilishwa na viongozi wa TANAPA na wanazuoni maarufu akiwemo Nd.
Jenerali Ulimwengu na Dkt. Alfred Kikoti. Inatarajiwa kuwa washiriki watapata
fursa ya kuchangia na mwishoni watatushauri namna ya kuboresha utekelezaji wa
majukumu yetu",alisema Kijazi.
Mkurugenzi wa Utalii na Masoko TANAPA,Bwa.Ibrahim Mussa akifafanua jambo katika Warsha ya siku tatu ya Wahariri wa Habari na Wana habari kutoka vyombo mbalimbali,inayofanyika jijini Mwanza katika hotel ya Gold Crest. Kauli mbiu ya Mkutano
wa mwaka huu ni “Wajibu wa Vyombo vya Habari katika kukuza utalii”. Pamoja na
kuelezea shughuli za TANAPA,aidha imeelezwa katika Warsha hiyo kuwa mada zitakazowasilishwa zitahusu masuala ya Utalii
na Uhifadhi na namna wanahabari wanavyoweza kushirikiana nasi katika kuhimiza
uhifadhi na kuendeleza utalii.


Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa
(TANAPA),Ndugu Allan Kijazi pichani kati na Meneja Uhusiano wa Shirika la
Hifadhi za Taifa nchni (TANAPA),Pascal Shelutete akizungumza jambo
na Mkurugenzi wa Utalii na Masoko TANAPA,Bwa.Ibrahim Mussa katika Warsha
ya siku tatu ya Wahariri wa Habari na Wana habari kutoka vyombo
mbalimbali,inayofanyika jijini Mwanza katika hotel ya Gold Crest. Kauli
mbiu ya Mkutano wa mwaka huu ni “Wajibu wa Vyombo vya Habari katika
kukuza utalii”.
Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa nchini
(TANAPA),Pascal Shelutete akifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa
kwenye semina hiyo mapema leo asubuhi jijini Mwanza.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...