Katika jitihada zinazofanywa na Uongozi wa Jeshi la Magereza katika kujenga na kudumisha mahusiano baina ya Askari na Maafisa wote wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, tarehe 22 Juni, 2015 saa 3:00 asubuhi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest J. Mangu(pichani) anatarajia kufunga Mafunzo ya Uongozi wa Magereza Daraja la Pili, katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, Jijini Dar es Salaam.
Mafunzo hayo ambayo yamechukua muda wa miezi minne yalilenga kuwaandaa Maafisa kuwa viongozi wa kati katika vituo vya Magereza nchini. Jumla ya wahitimu ni 216, kati yao Wanaume 161 na Wanawake 44 wanatoka Tanzania Bara, na Wanaume 10 na Mwanamke 01 wanatoka Vyuo vya Mafunzo Zanzibar.


Sherehe hizo, zitajumuisha mambo yafuatayo:-

* Mgeni Rasmi kukagua Gwaride rasmi lililoandaliwa na wahitimu hao;
* Mgeni Rasmi kutoa vyeti kwa Wanafunzi waliofanya vizuri katika Mafunzo ya darasani na
  Mafunzo ya mbinu za medani;
* Mgeni Rasmi kuvisha cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Magereza kwa wahitimu wawili kwa niaba
  ya wahitimu wengine na;
* Mgeni Rasmi kutoa Hotuba.
Sherehe za ufungaji wa Mafunzo hayo zinatarajia kukamilika saa 8:00 mchana. Vyombo vya Habari vinakaribishwa kwenye sherehe hizo siku ya Jumatatu tarehe 22 Juni, 2015 kuanzia saa 3:00 asubuhi.
Imetolewa na;
                      Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza;
                      Afisa Habari wa Jeshi la Magereza nchini;
                      Makao Makuu ya Jeshi la Magereza;
                      DAR ES SALAAM
                      Juni 19, 2015.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...