Mkuu wa wilaya ya Mufindi Bi MBONI MHITA amewataka wakazi wa mkoa wa
Iringa kuhakikisha wanakuwa walinzi namba moja dhidi ya watu wenyetabia ya
kuharibu mazingira katika maeneo yao, kwani kwa kutofanya hivyo ni sawa na
kujiuwa wenyewe.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya habari na mawasiliano ya Halmashauri ya wilaya ya
Mufindi Imetanabasha kuwa, mkuu wa wilaya ameyasema hayo kwenye kilele cha
siku ya mazingira duniani yaliyofanyika kimkoa katika kijiji cha Vikula Wilayani
Mufindi Mkoani Iringa alipomwakilisha mkuu wa Mkoa kama mgeni rasmi.
MHITA amesema endapo wananchi hawata chukua hatua dhidi ya watu wenye
tabia ya za kuvuna miti kiholela, ufugaji wa mifugo usiozingatia taratibu za
kitaaluma, uchomaji moto ovyo, uharibifu wa vyanzo vya maji, uwindaji haramu
na ukataji mijti ovyo, kunauwezekano mkubwa wa kutoweka kwa misitu na
vyanzo vya maji nchini na kuhatarisha ustawi wa mwanadamu.
Aidha, ameyataja madhara yanayotokana na uharibifu wa mazingira kuwa ni
pamoja na mbadiliko ya hali ya hewa, kuongezeka kwa hewa ya ukaa, misitu
kuteketea kwa moto, kupungua kwa kiasi cha mvua na majra yake kubadilika
kuongezeka kwa joto sanjari na kupungua kwa mavuno mashambani.
Kaulimbiu ya siku ya mazingira mwaka huu inasema ndoto bilioni saba. Dunia
moja . Tumia rasilimali kwa uangalifu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...