FAMILIA YA ELISA  NA ADELITA NYITI WA KILUVYA/KIBAHA TANZANIA WANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MTOTO WAO EMMANUEL NYITI. KILICHOTOKEA KANSAS CITY USA, SIKU YA JUMAMOSI TAREHE  06/20/2015.


HISTORIA FUPI  YA MAREHEMU
Emmanuel Elisa Nyiti alizaliwa  March 21, mwaka  1973 mkoani Dar es Salaam Tanzania kabla  ya mauti kumfikia Juni 20 mwaka 2015.



Elimu ya awali aliipata katika shule ya msingi Kibaha  na baadaye akajiunga na shule ya sekondari Kibaha kutoka mwaka 1987 mpaka 1990.



Baada ya kumaliza Kidato cha Nne alijiunga na sekondari ya Iliboru, Mkoani Arusha kwa elimu ya Kidato cha Tano na cha Sita. Kutoka mwaka 1991 mpaka 1993 .
 Mwaka  1994  Emmanuel alijiunga na chuo cha Ardhi  Dar es Salaam na mwaka  2000, Emmanuel  alijiunga na Butler Community College Eldorado Kansas, USA.



Mwaka  2002, Emmanuel aliondoka Wichita Kansas na kuhamia  Kansas City Missouri mpaka hapo kifo kilipomfika. Emmanuel  atakumbukwa na wengi sana kwa ucheshi, upole  na ushirikino wake mzuri na Watanzania wenzake .



Kwa Minnesota, tafadhali wasiliana:
Riwa Obel :  952-457-0599
Mchungaji A. Mwalilino:  763-496-9292
Ndaga Mwakabuta:  612 720-1791
Erick Lemunge:  651-398-1861
Amide Mutaboyerwa: 952-200-9743
Soga Mbilima:  612-865-2500
Elia Aswan:  651-325-6882
Jeremiah Balisidya:  763 516 4064
Jackson Molel  : 651-334-0163



Kwa Kansas. City Missouri  community
Please contact :
John Adhero (316) 644 0828
Dan Muro (913) 980-1116
Maura Limihagati (816) 456-0969
Fred Mwisomba (913) 244-3584
Peter Marara (913) 636-2675



Kwa michango tumia akaunti ifuatayo:
Jina: Ainassa Nyiti
Benki: Wellsfargo
Akaunti #: 396 046 9926

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 23, 2015

    Kwa kweli nimesikitika sana. Emmanuel nilisoma nae Ilboru miaka hiyo. Alikuwa kijana mfupi na maji ya kunde. Ni kweli alikuwa mtu mcheshi mcheshi. Tangu enzi hizo sikupata kuonana naye tena. Nini kimempata katika mwaka wake wa 42 tu? Wana-Ilboru mbona tunaondoka hivi jamani? Mwaka jana nilisoma humu pia kuwa Robert Mshomi kaondoka. Sasa zamu ya Nyiti! Tujiandae jamani. Poleni sana wazazi, ndugu, jamaa na marafiki. Katangulia, sote tutamfuata.

    ReplyDelete
  2. Gadiel Minja and familyJune 23, 2015

    Poleni sana Ainasa, Frida na mama kwa msiba huu. Mwenyezi Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu mno! May the Lord grant eternal peace to our beloved Emmanuel's soul. Rest in Peace Emmanuel!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 24, 2015

    R.I.P kaka Emmanuel

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...