Mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Muslim Hassanali akirudisha fomu kwa Mratibu wa Kanda ya Pwani, Casimir Juma Mabina za kuomba kuteuliwa kuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya chadema katika uchaguzi mkuu ujao. Kulia ni Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema, Mabere Marando. (Picha na Francis Dande)
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mabere Marando (kushoto) akimkabidhi kadi ya Chama hicho aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM tawi la Kigamboni Wilaya ya Mafia, Mohamed Makungu ambaye amekiama chama chake na kujiunga na Chadema. Hafla hiyo ilifanyika katika Ofisi za Kanda ya Pwani jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mwenyekiti Bodi ya Wadhamini wa chama hicho, Arcado Ntagazwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...