Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini Arusha Mustafa Panju akiongea na vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake ,akitangaza rasmi kuwania kiti cha ubunge jimbo la Arusha mjini kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM
 Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Bushbucks Safaris iliyopo jijini Arusha Mustafa Panju akiongea na vyombo mbalimbali vya habari ofisini kwake ,akitangaza rasmi kuwania kiti cha ubunge jimbo la Arusha mjini kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM kushoto ni mke wake
 Kassim Mamboleo ambaye ni katibu wa kamati ya ushindi ya mgombea Mustafa Panju akitoa utambulisho kwa vyombo vya habari
Taswira katika mkutano huo na waandishi wa habari

Na Pamela Mollel, Arusha
JIMBO la Arusha ni moja ya jimbo ambalo linaonekana kuwa  ni jimbo lenye siasa komavu, kutokana na hali hiyo limeonekana kuongoza kwa vurugu na uvunjifu wa amani , ambapo kupitia kwa Mtangaza nia wa ubunge jimbo la Arusha mjini  Mustafa Panju amewahakikishia wananchi
kurudisha amani hiyo.

Jimbo hilo ambalo linashikiliwa na Mbunge wa Arusha mjini kupitia 
chadema ,Godbless Lema ambaye hivi sasa ametangaza tena kulitaka jimbo 
, ambapo hadi hivi sasa jumla ya wagombea 18 kupitia chama cha
mapinduzi wamejitokeza kumg’oa mbunge huyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana  wakati akitangaza nia ya 
kuwania ubunge kupitia chama cha mapinduzi , Panju alisema kuwa ipo 
sababu ya kurudisha jimbo hilo mikononi mwa CCM kwa kuwa CCM ni chama
kinachopenda amani na kinachodumisha amani.

‘kila mmoja anatambua jinsi ambavyo jiji la Arusha hivi sasa halina 
amani kabisa na hakuna mtu anayedhubutu hata kutembea usiku , ila 
nitahakikisha linakuwa jiji la amani na utulivu na kuwawezesha 
wananchi wake kufanya shughuli zao bila hofu yoyote’alisema Panju.
Alifafanua zaidi kuwa,mbali na kurejesha amani jijini Arusha
atahakikisha anaondoa makundi mbalimbali yaliyopo miongoni mwa 
wananchi kwa kuwafanya wawe wamoja na wenye ushirikiano ili kuleta 
mabadiliko katika jimbo la Arusha kwa ujumla.
Pia alisema kuwa,wagombea wote wa nafasi ya ubunge katika chama ni 
wajibu wao kujenga Undugu,Upendo, na urafiki wakati wote ili kuepuka 
kujenga makundi ndani ya chama kwa misingi mbalimbali ya ukabila, 
udini na hata urangi.
Panju alisema kuwa, swala la kuwepo kwa makundi na vikundi katika 
vyama na kwa wananchi linapaswa kuangaliwa kwa umakini kwani 
likiendelea kuwepo linajenga uhasama ndani ya chama  na pia uhasama
unaoleta ubaguzi ndani ya nchi kwa ujumla 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 22, 2015

    Panju bana wewe umepita bila kupingwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...