Uhakiki wa vikundi vya vijana vilivyopewa msaada wa mashine na NHC ili kujiajiri na kusaidia wananchi kupata matofali ya kujengea nyumba bora umeanza katika Mikoa mbalimbali ukianzia na Mkoa wa Lindi na Mtwara. Katika hali isiyotarajiwa Mkoa wa Mtwara ambao kwa muda mrefu umekuwa ukililia kuletewa maendeleo umeshindwa kutumia fursa ya msaada wa mashine kwa vijana waliyopewa na NHC hali iliyolifanya Shirika kutwaa baadhi ya mashine ili zipewe vikundi vingine vinavyofanya vizuri Fuatilia kupitia habari picha hizi ili ufahamu kilichojiri katika mikoa hiyo ya kusini mwa Tanzania. Leo uhakiki huo unaendelea Mkoani Ruvuma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa Bw. Nicholous Kombe akimsikiliza Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC Bw. Muungano Saguya akimshukuru kwa Halmashauri hiyo kusaidia kikundi cha vijana kwa kuwawezesha fedha na udongo kwa ajili ya kutengeneza matofaliya kufungamana. Katikati ni Meneja wa NHC Mkoa wa Lindi Bw. Mussa Patrick Kamendu.
Jengo la Ofisi ya kikundi cha vijana cha Narunye(hakuna kutegeana) katika Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini likiwa limeonwa na Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kama inavyoonekana. Kikundi hiki kimeshaanza kupata maombi mengi ya matofali kutoka kwa wananchi wanaohitaji.
Kikundi cha vijana cha Ruangwa Materials Group katika Halmashauri ya Wilaya Ruangwa kimeshatengeneza matrofali kwa kutumia mashine ya msaada kutoka NHC. Halmashauri ya Wilaya hiyo imeamua kuyatumia matofali ya vijana hawa kujengea zahanati na majengo mengine yanayohitajika katika Halmashauri zikiwemo nyumba za Waalimu.
Meneja wa NHC Mkoa wa Lindi Bw. Mussa Patrick Kamendu akitoa mawaidha kwa kikundi cha vijana cha Narunye kilichopo katika Wilaya ya Lindi vijijini baada ya kutembelea kikundi hicho kukagua kazi zake.Vijana hawa wanajihusisha pia na utunzaji mazingira.
Baada ya Wakurugezi wa Halmashauri za Kilwa na Lindi Vijijini kutokuwa karibu na vikundi vya vijana, Meneja wa Huduma kwa Jamii wa NHC na Meneja wa Mkoa wa Lindi waliweza kufanya mazungumzo nao ya kina na hatimaye wamekubali kuwasaidia vijana waliopewa msaada wa mashine na NHC katika Halmashauri zao ili waweze kujiajiri. Kulia ni Bi. Oliver Vavunge ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Vijijini na wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kilwa Bi. Maimuna Mtanda.
Vijana Mtwara wahamasishwe kuchangamkia fursa za kufyatua matofali huu sio wakati wa kuchagua kazi.
ReplyDelete