SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) limeboresha huduma kwa wateja wake kwa kubadilisha muonekano wa ofisi zake za jijini Dar es Salaam ili kupunguza urasimu wa kutoa huduma sanjari na utaratibu wa wateja kubonyeza kitufe maalum kwaajili ya maoni ya huduma zinazotolewa.

Aidha sekta isiyo rasmi na rasmi zimeaswa kujiunga na mifuko ya hifadhi ya jamii itakayowawezesha kujikwamua kiuchumi kwani waliojiandikisha kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii ni wachache hali inayopelekea wazee kujiingiza katika ulinzi .

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha hivi karibuni.

Alisema lengo la kuboresha ofisi hizo ni kuhakikisha wateja wanapata kile wanachokihitaji sambamba na kuondoa msongamano wa kupata huduma mbalimbali zinazotolewa na mfuko huo lakini pia wamekuja na huduma nyingine muhimu kwaajili ya kupima utendaji kazi kwa wafanyakazi wanaowahudumia wateja.

Alisema sababu nyingine ya kuboresha ofisi za Dar es salaam ni kutokana na kuwa na wachama wengi ambapo asilimia 75 ya wanachama wa Mfuko huo wapo huko.

“Lakini tukishamaliza huko tutaenda mikoa mingine kuboresha ofisi na mazingira ya ofisi yawe mazuri, ili wateja wapate huduma bora na za uhakika”.

Akizungumzia suala zima la sekta isiyo rasmi na rasmi ni vyema kujiunga katika mifuko hiyo ya jamii ili waweze kujiwekea akiba na baadaye kunufaika na mafao mbalimbali kwani vijana hivi sasa wanafariki na kuwaacha wazee hali inayopelekea wazee kukosa misaada kwa tegemezi wao na kusababisha kuingia katika sekta mbalimbali ili waweze kupata fedha za kijikimu na maisha.

“wazee hivi sasa ndio wanabaki na vijana ambao ni tegemezi wanakufa hivyo ni vyema sasa kuhakikisha watu wanajiunga na mifuko ya hifadhi za jamii na kuboreshwa maisha yao “.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea juu ya Shirika lilivyojipanga kuboresha huduma za wateja wake.
Mkuu wa Idara ya Masoko na Uhusiano wa NSSF, Eunice Chiume akionyesha kifaa maalum cha  maoni ya Wateja wa NSSF juu ya huduma wanazozitoa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...