THE
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE
HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete ametuma
salamu za rambirambi kwa Waislamu wote nchini na Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania (BAKWATA)) kufuatia kifo cha Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti
Sheikh Issa Bin Shaaban Simba.
Marehemu Mufti amefariki leo
15/6/2015 asubuhi katika hospitali ya TMJ – DSM alipokuwa amelazwa akisumbuliwa
na ugonjwa wa sukari na shinikizo la damu (pressure).
"Kifo kinaleta huzuni,
hata hivyo Kifo hakizuiliki, hatuna budi kukikubali na ni wajibu wetu kumuombea
Sheikh Mkuu kwa Mola wetu ampe mapumziko ya milele". Rais Kikwete ametuma salamu hizo za rambirambi kupitia kwa
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum.
"Nawaombea subra wana familia, ndugu, jamaa, waislamu wote
na wana jamii kwani Mufti alikua kiongozi katika Jamii yetu'” Rais
amesema na kueleza kuwa "Kamwe
mchango wake hautasahaulika katika jamii yote kwa Ujumla na hakika sote
tutamkumbuka" ameongeza.
Marehemu alijiunga na BAKWATA mwaka
1968 na amekuwa mwalimu wa chuo katika mikoa mbalimbali ya Mwanza, Bukoba na
Mwaka 1970 alikuwa Shekhe wa Mkoa wa Shinyanga.
Rais amemuelezea Marehemu Mufti kama
mwalimu katika jamii ambaye alikua na uzoefu wa hali ya juu na mwenye kupenda
dini yake na kuitumia kwa manufaa ya jamii iliyomzunguka
"Amekua mwalimu imara
na mtu wa kutumainiwa na kutegemewa katika uislamu na jamii kwa ujumla, hakika
tutamkumbuka siku zote' Rais Kikwete ameongeza.
Shekhe Issa Bin Shaaban Simba alikuwa
na uzoefu mkubwa ndani ya BAKWATA na aliwahi kukaimu nafasi ya
mufti kwa siku 90, baada ya kifo cha Mufti Hemed mwaka 2002.
Baada ya hapo akasimamia mchakato wa uchaguzi
wa Mufti Mkuu na baadaye 2003 akachaguliwa kuwa Mufti Mkuu wa Tanzania.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yake
pahali pema Peponi, Amina.
Imetolewa na :
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu-DSM
15 Juni, 2015
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...