Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
akikaribishwa na Waziri Mkuu wa India, Mheshimiwa Narendra Modi mara baada ya
kuwasili Ikulu ya India kwa sherehe za ukaribisho wake rasmi nchini India kwa
ajili ya ziara yake ya Kiserikali. Sherehe hizo zimefanyika asubuhi ya leo,
Ijumaa, Juni 19, 2015.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete, Waziri Mkuu wa
IndiaMheshimiwa Narendra Modi, na Rais Wa IndiaMheshimiwa Pranad Mukherjee
wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi baada ya Rais kikwete kuwasili katika
ikulu ya India kwa mapokezi rasmi(picha
na Freddy Maro).
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akikagua
gwaride la Majeshi ya India liliandaliwa kwa ajili ya kumkaribisha kwa ziara
rasmi ya Kiserikali nchini India katika sherehe za ukaribisho zilizofanyika
asubuhi ya leo, Ijumaa, Juni 19, 2015.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiagana
na Rais wa India, Mheshimiwa Pranad Mukherjee (kushoto) na Waziri Mkuu,
Mheshimiwa Narendra Modi mara baada ya kumalizika kwa sherehe za kumkaribisha
nchini India kwa ziara rasmi ya Kiserikali. Sherehe hizo zimefanyika Ikulu ya
India mjini New Delhi, asubuhi ya leo, Ijumaa, Juni 19, 2015.
(Picha na Freddy Maro)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...