Katibu
Mtendaji wa Shirika lisilokua la kiserikali la ANGONET lenye makao makuu
jijini Arusha ,Petter Bayo (kulia) akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) juu ya masuala ya lishe na kuitaka serikali iweke
vipaumbele katika
lishe ili kutokomeza matatizo ya udumavu na utapiamlo,Katikati ni Mratibu wa
Angonet ,Petro Ahham ,kushoto ni Jovitha Mlay mwanachama wa shirika
hilo(habari picha na libeneke la kaskazini
blog)
Serikali imetakiwa kuweka vipaumbele katika
masuala ya lishe
ili kutokomeza matatizo ya udumavu na utapiamlo yanayosababishwa na lishe duni
hivyo kuathiri maendeleo ya jamii na taifa kwa
ujumla.
Katibu Mtendaji wa shirika lisilokuwa la
kiserikali (ANGONET)
,Petter Bayo amesema kuwa kutokana na hali mbaya ya lishe nchini na kuongezeka
kwa udumavu wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano 5 hadi kufikia asilimia
42% ya watoto hao kwa mujibu wa utafiti uliofanyika mwaka
2012.
Bayo alisema hayo jana akizungumza na
Waandishi wa habari
amesema kuwa iwapo hatua za
makusudi hazitachukuliwa
athari zitakua kubwa katika shughuli za uzalishaji kutokana na lishe duni na
pia kuathiri Nyanja za elimu na sekta mbali mbali kuwa
hayo jana akizungumza na Waandishi wa
habari.
“Lishe ni kiini cha maendeleo ya jamii
yoyote ile na nchi
yoyote ile ni vyema serikali ikatilia mkazo suala la lishe kwani ni kichocheo
muhimu cha maendeleo kwa kuhamasisha na kutoa elimu kwa wananchi hasa waishio
vijijini” Alisema Bayo
Mratibu wa Angonet ,Petro Ahham alisema
kuwa Serikali
inapaswa kutupia macho suala la upatikanaji wa chakula na kuangalia uhaba wa
chakula unaoweza kusababisha watu kufa kwa kukosa
chakula.
Ahham anaeleza kuwa ukosefu wa madini chuma kwa watoto
umekua
ukisababisha ugonjwa wa Anemia unaowapelekea watoto kusinzia wakiwa mashuleni
hata kuchangia kushuka kwa kiwango cha ufaulu
kutokana na Lishe duni.
Mwanachama
wa Angonet ,Jovitha Mlay anaeleza kuwa shirika hilo kwa sasa linashirikiana
Umoja wa mashirika yanayojihusisha na masuala ya
lishe Tanzania (PANITA) katika kutoa elimu
juu ya lishe na kufanya uhamasishaji mashuleni na katika makundi mbalimbali ya
jamii husasan kwenye Kanda ya Kaskazini,mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na
Manyara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...