Waziri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya Salum (wa pili kulia) akiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dr. Servacius
Likwelile pamoja na Msajili wa Hazina, Nd. Lawrence Mafuru wakipokea hundi ya mfano ya shilingi
Bilioni 3 kutoka Kampuni ya Puma Energy Tanzania Limited iliyokabidhiwa na Mkuu wa Puma
Energy Tanzania Limited, Nd. Philippe Corsaletti.
Waziri wa Fedha, Mh. Saada Mkuya Salum akiwashukuru watendaji wakuu wa Puma Energy Tanzania
Limited kwa kuwasilisha kwa Serikali gawio la faida la shilingi Bilioni 3. Mawasilisho hayo yalifanyika
katika Ofisi za Wizara ya Fedha,Mjini Dodoma. Kulia kwa Mh.Waziri ni Dr.Servacius Likwelile,Katibu
Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...