Katibu Mkuu Wizara ya Afya na ustawi wa jamii Dk. Donan Mbando akiwa kwenye picha ya pamoja na madaktari na viongozi wa chuo kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi cha Muhimbili (MUHAS)  mara baada ya kufunga mkutano mkuu watatu wa sayansi ya afya uliondaliwa na chuo hicho jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita. Kushoto kwake ni Makamu mkuu wa MUHAS, Prof. Ephata Kaaya. 
 Katibu Mkuu Wizara ya Afya na ustawi wa jamii Dk. Donan Mbando akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa udaktari, madaktari na viongozi wa chuo kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi cha Muhimbili (MUHAS)  mara baada ya kufunga mkutano mkuu watatu wa sayansi ya afya uliondaliwa na chuo hicho jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya na ustawi wa jamii Dk. Donan Mbando akiagana na baadhi ya wanafunzi wa udaktari kutoka chuo kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi cha Muhimbili (MUHAS)  mara baada ya kufunga mkutano mkuu watatu wa sayansi ya afya uliondaliwa na chuo hicho jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

SERIKALI imewaomba watafiti wa masuala ya afya hapa nchini kuhakikisha kwamba wanaibua hoja mpya zitakazosaidia kuleta mabadiliko kwenye sera za kitaifa zinazohusu sekta hiyo muhimu. Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Katibu Mkuu Wizara ya Afya na ustawi wa jamii Dk. Donan Mbando mara tu baada ya kufunga mkutano mkuu watatu wa sayansi ya afya uliondaliwa na chuo kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi cha Muhimbili (MUHAS).

“Kwa sasa taifa linashuhudia ongezeko kubwa la idadi ya watu wanaosumbuliwa na magonjwa yasiyoyakuwa ya mbukiza kama vile kisukari, shinikizo la damu na kisukari. Kwa bahati mbaya sana vituo vyetu vingi vya afya havijaandaliwa vizuri kukabiliana na magonjwa haya kwasababu sera zetu wakati zinaandaliwa hazikujika zaidi kwenye magonjwa yasiyoyakuwa ya kuambukiza na ndio maana tunahitaji mabadiliko kwenye hili,’’ alisema Dr. Mbando.

Dr. Mbando alizataja sababu kubwa zinazochangia ongezeko la magonjwa hayo kuwa ni pamoja na matumizi ya pombe kupita kiasi, aina ya vyakula vinavyotumiwa na watanzania hususani wale wanaoishi maeneo ya mijini, kutokufanya mazoezi pamoja na uvutaji wa sigara. Aidha aliiongeza kuwa kwa sasa serikali ipo kwenye mpango wa kuandaa mkakati  wanne wa huduma za afya hapa nchini (health care financing strategy) utakao muwezesha kila mtanzania kuwa na bima ya afya. 

“Kwa sasa ni asilimia 20 tu ya watanzania ndio wanamiliki bima za afya zinazotolewa na shirika la bima ya afya la taifa na mashirika binafsi na hivyo kufanya asilimia 80 ya watanzania kuishi bila kuwa na uhakika wa masuala ya tiba….hili tumelianza tayari,’’ alibainisha.

Kuhusu mlipuko wa ugonjwa wakipundupindu kwenye mikoa ya kagera na kigoma uliosababishwa na kuingia kwa wakimbizi kutoka Burundi, Dr. Mbando alisema kwa sasa serikali kwa kushirikiana na Wananchi, wadau wa maendeleo na asasi zisizo za kiraia wanapambana kuhakikisha tatizo hilo linakwisha.

Akizungumza kwenye mkutano huo Makamu mkuu wa MUHAS, Prof. Ephata Kaaya alisema kwa sasa taifa linahitaji zaidi tafiti za kiafya hususani kwenye magonjwa yasiyo ya kuambukiza na ndio sababu mkutano huo ulijikita zaidi kujadili tatizo hilo. 

“Kama wataalamu wa masuala ya afya tunaona kuna haja kubwa tukiwekeza katika tafiti zinazolenga kuibua changamoto na suluhisho kwenye magonjwa haya,’’ alisema. Mkutano huo wa siku mbili ulihudhuriwa na washiriki zaidi ya 300 wakiwemo madaktari, viongozi na wanafunzi wa udaktari kutoka MUHAS na vyuo vingine vya afya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 02, 2015

    Kampeni za afya zilikuewepo toka wakati wa uhuru ziendelee kila mahali ili tuimarishe afya zetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...