Mwanasiasa mkongwe nchini, Sir. George Kahama akizungumza na wana CCM na wakazi wa Lindi katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana, wakati Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (wa tatu kushoto waliokaa), alipotangaza nia ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba, katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana. Wengeni (kutoka kushoto) ni Katibu wa CCM Mkoa wa Lindi, Adelina Gefi na Mke wa Waziri Membe, mama Dorcas Membe.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe (kushoto), akimpongeza Mwanasiasa mkongwe nchini, Sir. George Kahama baada ya Mzee Kahama kuhutubia umati wa  wana CCM na wakazi wa Lindi katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoa jana, wakati Mheshimiwa Membe alipotangaza nia ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba.


Mama Dorcas Membe mke wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Bernard Membe, akimpongeza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Lindi, Mzee Ali Mtopa baada ya kuhutubia umati wa  wana CCM na wakazi wa Lindi katika Viwanja vya Ofisi ya CCM Mkoani humo jana, wakati Mheshimiwa Membe (katikati), alipotangaza nia ya kugombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Mwezi Oktoba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 08, 2015

    mbona Sir.kahama hashutumiwi kama alivyoshutumiwa kingunge alipomunga mkono Lowasa.Usawa uko wapi hapa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...