Na Avila
kakingo,Globu ya jamii.
KAMPUNI ya
Solution BLOCKS ikishirikiana na kampuni ya Anglo Gold Ashanti waandaa mkutano
wa Alhamisi ya kila mwezi ili kushirikisha taasisi mbalimbali za serikali na zisizo za
kiserikali kuzungumzia kuchangia katika maendeleo katika jamii.
Hayo
yamesemwa na Makamo wa Rais wa Sustainability Aglo Gold Ashanti, Simon Shayo
katika ufunguzi wa mkutano ambao umejulikana kwa jina la THURSDAY TALK uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam jana.
Nae Mkurugenzi
Mkuu wa kampuni ya Solution Blocks (Facilitator), amesema kuwa Makampuni na
taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali lazima ziwajibike na kuelemisha
jamii pia na kutoa fursa kwa wadau wa maendeleo hapa nchini ili kushiriki vyema
katika kuleta maendeleo.
Pia ametoa
wito kwa makampuni, NGO, taasisi za Serikali pamoja na Asasi za kiraia kuwajibika
kushiriki vyema katika kuleta maendeleo
ya elimu,Afya,mazingira, maji pamoja na utawala bora katika taasisi hizo.

Makamu wa Raisi-Sustainability Anglo Gold Ashanti-Mgodi wa Geita,, Simon Shayo akizungumza na wadau waliohudhuria katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam jana kuhusiana na mgodi wa dhahabu wa Geita jinsi unavyofanya kazi zake na kulinda afya za wananchi wa maeneo hayo ili wasidhurike na uchimbaji wa madini hayo.
Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa Anglo Gold Ashanti -Mgodi wa Geita, Tenga .M. Tenga akizungumza katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam jana ulioandaliwa na kampuni ya Solution Blocks.
Baadhi ya wadau waliohudhuria katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam jana kampuni ya Solution Blocks.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...