Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
Watoto wametakiwa kujaliwa kwa kila namna ili kuwaanda kuwa taifa bora kutokana na misingi ambayo imewekwa kwa watoto hao.
Akizungumza na leo katika maadhimisho ya kuezi kuzaliwa kwa mwanzilishi Vijiji vya Watoto SOS,Herman Gmeiner,Mkurugenzi wa Kijiji cha SOS,Anglolwisye Mwollo-ntalima,amesema kuwa kila juni 23 kila mwaka wanaadhimisho kuzaliwa kwa Gmeiner.
Mwollo-ntalima amesema kuwa kutokana na mwanzilishi huyo kwa sasa Rais wa SOS ni mtu aliyetokana na SOS na kizazi hicho kinaendelea kuwepo.
Amesema kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni Nijali mimi ambayo dunia nzima imeadhimisha siku hiyo kwa kumkumbukA Mwanzilishi wa SOS.
Katika maadhimisho ya SOS ,Kampuni ya Kontena ya Maersk Line imetoa msaada wa komputa katika kijiji cha watoto ili waweze kutumia kutokana na ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano.
Mkurugenzi wa Maersk Line,Morten Juul amesema anatambua kazi inayofanywa na SOS katika kuwatunza watoto kwa unagalifu.
Mkurugenzi wa kijiji cha watoto cha SOS hapa nchini, Angolwisye Mwollo-Ntallima akicheza na watoto katika siku ya maadhimisho ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa SOS duniani,ambayo hufanyika kila Juni 23 kila mwaka, iliyofanyika katika kijiji cha SOS- Ubungo jijini Dar es Salaam leo.
Mwalimu mkuu wa watoto wadogo wa kituo cha SOS ,Agnes Mlema akizungumza leo katika siku ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa kwa mwanzilishi wa SOS duniani,ambayo hufanyika kila Juni 23 kila mwaka, iliyofanyika katika kijiji cha SOS- Ubungo jijini Dar es Salaam leo. 
Baadhi ya watoto wakicheza ngoma leo katika kituo cha kulelea watoto yatima cha SOS Ubungo jijinio Dar es Salaam.
Nkurugenzi mkuu wa Maersk Line, Morten Juul akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto wa kituo cha SOS pamoja na viongozi wa kituo hicho baada ya kutoa msaada wa kompyuta katika kituo hicho leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Chalila Kibuda Globu ya jamii)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...