Sehemu ya kundi kubwa la familia ya simba linaloishi pamoja maarufu kama "Super Pride" likiota jua katikati ya Mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Kundi hili, ambalo aghalabu huwa na wanafamilia wapatao 21, huishi pamoja na kutumia muda mwingi kuwinda na kulinda kinda wao ambao huwa katika hatari ya kuliwa na wanyama wadokozi kama vile fisi, na wakati mwingine madume ya Simba wanaotaka kuingia kundini kwa nguvu. Mara nyingi mmoja wa wanafamilia wa kundi hili hufungwa redio shingoni na watafiti wanaofuatilia tabia na nyendo za mfalme huyu wa mwituni.
Home
Unlabelled
Super Pride
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Picha ya simba imependeza, tujivunie na kukuza utalli nchini, vivutio vya utalii viko vingine na katika sehemu nyingi za nchi yetu ni kujipanga to kuhakikisha vinaendelezwa ili kuongeza mapato nchini na kuwawezesha wakulima wafanyabiashara na vyombo vya usafiri kunufaika na uchumi huu utakaoongezeka. Mikoa yetu yenye mwambao wa pwani ina uwezo wa kutengeneza fursa nzuri za utallii wa nje n ndani wakiboresha maeneo yao na huduma.
ReplyDelete