Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikilia watu saba kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya uhalifu ikiwa ni pamoja na unyang’anyi wa kutumia silaha. Watuhumiwa wamekamakwa katika matukio tofauti jijini Dar es Salaam kufuatia oparesheni kali inayoendelea ya kuwasaka wahalifu wa makosa mbalimbali.
Katika tukio la kwanza mnamo tarehe 03/06/2015 majira saa 08:00HRS maeneo ya Tabata Kinyerezi mtaa wa Kibaga askari wa kikosi kazi (TASK FORCE) walimkamata mtuhumiwa HEMED S/O HASSAN MRISHO @ BUDA, Miaka 31, Mfanyabiashara, Mkazi wa Tabata Kinyerezi, akiwa na Bunduki aina ya SMG iliyofutwa namba zake ikiwa na risasi 10. Mtuhumiwa alikamatwa kufuatia taarifa toka kwa msiri kuwa anajihusisha na uhalifu wa kutumia silaha. Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mtuhumiwa HEMED S/O HASSANI akishirikiana na wenzake ambao wanasakwa, wanajihusisha na unalifu wa kutumia silaha. Atafikishwa mahakamani mara uchunguzi utakapokamilika.
Katika tukio lingine, mnamo tarehe 01/06/2015 majira ya saa 02:00 huko maeneo ya Tegeta Mashimo ya Kokoto, Polisi walifanikiwa kukamata risasi 49 za bunduki aina ya Short Gun zikiwa katika mfuko wa Rambo baada ya kuwakurupua vijana wanaokaa katika vijiwe vya mashimoni hayo.
Hii ni kufuatia kundi la vijana wanaokadiriwa kufikia kumi wakiwa na mapanga na silaha nyingine za jadi kuvamia nyumba ya VERONICA D/O SABATH MAMBOYA na kuiba vitu mbalimbali vikiwemo vitambulisho, TV, Laptop na Pesa taslim TSHS. 300,000/=. Baada ya tukio mlalamikaji alitoa taarifa kituo cha polisi Kawe na ufuatiliaji ulianza mara moja. Polisi walifanikiwa kuwakamata vijana watatu ambao walionyesha vijiwe vya vijana wenzao.
![]() |
Naibu Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam (DCP), Simon Sirro akiwaonesha risasi zilizokamatwa katika oparesheni hiyo. |
kazi nzuri. asanteni.
ReplyDelete