
Akitolea
ufafanuzi wa takwimu hizi Bwana Vernon Frye, Mkuu wa Usalama mitandao wa
kampuni ya Vodacom ya Afrika kusini, alielezea kuhusiana na uhalifu mpya wa
Ransomware ambapo tayari athari zake zimesha onekana Nchini huku aki ibua
mjadala mzito wa wapi tume jikwaa.
Aidha
Mjadala mrefu kutoka kwa aliyekua Mkurgenzi wa wakala wa usalama wa Marekani
(National Security Agency – NSA) bwana William Binney pamoja na Raisi na
muanzilishi wa kivinjari cha aina ya Tor kinachotumika sana na jumuia ya wana
usalama mitandao waliibua changamoto ya ufaragha baina ya watumiaji wa mitandao
na namna ya kuendelea kuhakiki kunapatikana uthibiti wa faragha hizi kutotumika
vibaya na wahalifu.
Nikiwasilisha
mada ya changamoto tulizo zazo barani Afika na nini kifanyike ili kujikwamua
katika hali mbaya tuliyo nayo hivi sasa ya wimbi la uhalifu mtandao barani
afrika ambapo umeendelea kugharimu bara katika Nyanja za kisiasa, kijamii
pamoja na kiuchumi. Nilielezea kwa kina mambo ya msingi tunayo takiwa kuyafanyia
kazi ili kuhakiki Bara linabaki salama.
Katika
mjadala huu ambapo wanausalama mtandao kutoka maeneo mbali mbali ya dunia
waliunga mkono nilicho zungumza kua bado kuna kusua sua katika ushirikiano wa
pamoja katika kutokomeza uhalifu mtandao huwa wahalifu mtandao kuonekana
niwenye ushirikiano ulimkubwa kabisa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...