Na Dotto Mwaibale
Marehemu  Ramadhani Kibanike enzi za uhai wake.
KAMPUNI ya JL Comunications inayochapisha magazeti ya Jambo Leo, Staa Spoti, imepata pigo baada ya aliyekuwa Meneja wake Mkuu Ramadhani Kibanike kufariki.

Kibanike amefariki dunia leo mchana nyumbani kwake Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam, baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Akitoa taarifa ya kifo hicho kwa wafanyakazi wa Kampuni hiyo, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Theophil Makunga alisema Kibanike alikumbwa na mauti jana mchana.

Taarifa hiyo ambayo iliwashtua wafanyakazi wa Kampuni hiyo na hata kupelekea baadhi yao kupoteza fahamu, ilisababisha pia kusimama kwa muda kwa shughuli za Kampuni hiyo.
Mipango ya mazishi bado inapangwa, na msiba upo nyumbani kwa marehemu Tabata Jijini Dar es Salaam. 
 Mhariri Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Julian Msacky na Mwandishi wa Habari, Stella Kessy (kulia), wakiendelea na kazi huku wakiwa na hudhuni baada ya kupokea taarifa ya kifo cha Kibanike.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...