Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Mkuu wa Idara ya magonjwa ya Tropiki Prof.Dr.med.Augustin Stich baada ya Taasisi ya Tafiti mbali mbali yakiwemo magonjwa ya Binadamu, Chuo cha Afya katika Mji wa Wurzburg kimeweza kutoa mchango mkubwa katikakupambana na maradhi ya Ebola yaliyotokea Nchi za Magharibi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakipata maelezo kutoka kwa Mario Gerth (kulia) wakati waalipotembelea katika kituo cha maonesho ya picha Spitale katika Mji wa Wurzburg picha hizo zenye kuonesha Zanzibar na Ustaarabu wa Waswahili zilizotayarishwa chini ya nusimamizi wa Dr.Stefan Oschman Mkurugenzi wa Tamasha la Muziki wa Afrika.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Mama Mwanamwema Shein (wa pili kulia) akiwa na ujumbe wake wakiangalia magari ya aina mbali mbali baada ya kupata maelezo kutoka kwa Adam Nowak M.A.Afisa anehusika na Ufundi wakati walipotembelea katika Kampuni ya Magari ya Mercedes-Benz na kuangalia magari hayo yaliyotayari kwa kuingia sokoni Mjini Wurzburg nchini Ujerumani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) na Mama Mwanamwema Shein (wa pili kulia) pamoja na Viongozi waliofuatana nao katika ziara ya kikazi Nchini Ujerumani wakiwa na ujumbe wake wakiangalia mashine ya gari aina ya Mercedes -Benz na kupata maelezo kutoka kwa afisa anaehusika na ufundi Adam Nowak M.A katika kampuni hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...